airtel

airtel

.

.

Thursday, December 21, 2017

WANAFUNZI 1,300 WA S/M NA SEKONDARI MKOA WA PWANI WAMEACHA SHULE KWA MWAKA 2014/2017-RC NDIKILO


IMG_20171208_111849
Baadhi ya viongozi na wadau wa elimu mkoani Pwani wakimsikiliza mkuu wa mkoa huo mhandisi Evarist Ndikilo ,wakati alipokuwa akizungumza masuala ya elimu na changamoto zinaxokabili sekta hiyo ,kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani
IMG_20171208_111648
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza jambo kuhusu masuala ya sekta ya elimu na changamoto inazozikabili kwa viongozi na wadau mbalimbali wa elimu mkoani hapo kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za jengo la mkuu wa mkoa . 
Picha na Mwamvua Mwinyi
…………..
Na Nurudini stambuli,Pwani
SERIKALI mkoani Pwani ,imeweka bayana kuwa,jumla ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari 1,300 wameacha shule (mdondoko),kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2014-2017,hali inayosababisha kukosa haki yao ya elimu.
Aidha kumekuwa na tetesi kwamba baadhi ya watoto hao wanaoacha shule hujihusisha na vikundi vya uhalifu ndani na nje ya mkoa huo ,jambo ambalo linahitaji nguvu za pamoja kulikomesha tatizo hilo.
Pamoja na hilo ,imeeleza kumekuwepo na tatizo la uzembe kwa baadhi ya wasimamizi wa elimu kutotekeleza ipasavyo majukumu yao,;:na pia kutofikiwa kwa malengo ya uandikishaji wa elimu ya awali na darasa la kwanza na udahili wa kidato cha kwanza hivyo kusababisha watoto wenye umri wa kwenda shule kutokwenda shule.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,aliyasema hayo wakati akizungumzia changamoto na masuala ya sekta ya elimu mkoa,kwa viongozi wa Idara ya elimu mkoani hapo, wakurugenzi,wakuu wa wilaya na wadau wa elimu.
Alielezea ,kati ya watoto hao 1,300 wanaodaiwa kuacha shule kwenye mkoa mzima ,kwa upande wa wilaya ya Rufiji ni wanafunzi 381 na Kibiti ni 110 .
“Niliwahi kuomba taarifa ya mdondoko kwa kipindi cha mwaka 2014-2017 kutoka kwa wakuu wa wilaya zote “
“Ambapo mkoa wa Pwani una jumla ya shule za msingi 613 na sekondari 174 ,ndipo nilipoletewa idadi hiyo ambayo kiukweli ni chanzo cha kuporomoko  kwa taaluma mkoani hapo” alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo aliagiza wanafunzi wote walioacha shule na watoro watafutwe ,warudishwe shule kisha wazazi na walezi wachukuliwe hatua za kisheria ikiwepo kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kufuatilia mahudhurio ya watoto hao.
Alibainisha lipo tatizo jingine la mimba kwa watoto wa kike ,upungufu na uchakavu wa miundombinu ya shule ikiwemo madarasa ,nyumba za walimu ,matundu ya vyoo,ofisi za walimu, maabara na hostel.
Mkuu huyo wa mkoa, alisema kwasasa shule za msingi kuna mahitaji ya vyumba vya madarasa 7,609 ,vilivyopo ni 4,010 hivyo upungufu ni madarasa 3,599.
Mahitaji ya nyumba za walimu ni 6,328 ,zilizopo ni 1,592 ,upungufu ni nyumba 4,736 ,matundu ya vyoo yanayohitajika ni 13,750 ,yaliyopo ni 5,375 upungufu ni matundu 8,375 .
Mhandisi Ndikilo alitaja mahitaji ya vyumba vya madarasa katika shule za sekondari mkoani Pwani kuwa ni 1,479 ,vilivyopo ni 1,366 ,upungufu ni 113 ,mahitaji ya nyumba za walimu 3,684 zilizopo 671 hivyo upungufu 3,013.
Matundu ya vyoo yanayohitajika ni 2,405 yaliyopo ni matundu 1,961,upungufu ni matundu 444 ,na mahitaji ya maabara ni 333 yaliyopo ni 195 na upungufu ni 138.
Hata hivyo ,Mhandisi Ndikilo alizitaka halmashauri mkoani humo ,ziande mkakati wa kujenga hostel katika kila shule ya sekondari ili kuwalinda watoto hasa wa kike wanaotembea umbali mrefu kwenda na kurudi shule.
Sanjali na hilo ,ziwe na mpango mkakati wa kujenga na kukarabati miundombinu ya shule ikiwemo vyumba vya madarasa ,matundu ya vyoo na nyumba za walimu na kukamilisha ujenzi ifikapo 2020 .
Alitoa wito kwa wadau wa elimu kuunga mkono juhudi za serikali ya mkoa katika ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari.
Katika hatua nyingine ,mhandisi Ndikilo alisema lengo la serikali ni kuimarisha sera ya viwanda ili kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ,na msingi mkubwa wa sera hiyo ni elimu.
Aliwataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi, watendaji wa halmashauri pamoja na watendaji wengine kuhakikisha wanafunzi wanaodahiliwa kidato cha kwanza wanasimamiwa hadi wanamaliza kidato cha nne ili waweze kushiriki katika kuimarisha uchumi wa viwanda.
Alisema kwamba,watoto wasipopewa elimu ,maarifa na ujuzi mahsusi watakuwa watazamaji badala ya watendaji licha ya mkoa huo kusheheni viwanda.

Wednesday, December 20, 2017

RAIS MAGUFULI ABAINI MADUDU KATIKA MKATABA WA AIRTEL NA TTCL

https://2.bp.blogspot.com/-CYppl-tNjgM/WjpA7lPvqlI/AAAAAAABp9s/CaWVv2rCWgMTyDew-mIx-QKFi2xq7ndHQCLcBGAs/s1600/1.jpg 
 RAIS John Magufuli amesema Serikali imebaini kuwa kampuni ya Mawasiliano ya Bharti Airtel ni mali ya Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL) na amemwagiza Waziri wa fedha na mipango kufuatilia suala hilo haraka ili Airtel irudishwe kumilikiwa na serikali.Rais ameyasema hayo leo Desemba 20 wakati akizungumza kwenye Ofisi za Taifa za Takwimu mjini Dodoma.“Kampuni ya AIRTEL imethibitika kuwa ni mali ya Shirika la TTCL, lakini kuna mchezo ulifanyika, sasa sitaki kuongea sana. Nataka Waziri wa Fedha ufuatilie suala hili kabla ya mwaka huu kuisha,” amesema Magufuli.Taarifa na ndani zinabainisha kwamba hisa za Airtel zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kuendesha biashara za kampuni hiyo yenye wateja wengi zaidi nchini ikiwa nyuma ya Vodacom na Tigo.Chanzo cha mpango huo kinatajwa kuwa ni uongozi wa juu wa TTCL uliotaka Serikali kudai haki zake za uwekezaji ndani ya Airtel ambako inaimiliki kwa ubia wa asilimia 40 kwa 60 na mwekezaji.Taarifa zinaarifu kuwa TTCL itamiliki hisa zote za Airtel Tanzania Limited ambapo tayari TTCL imewasilisha hoja ya kutaka kufanya hivyo baada ya kubaini kwamba Serikali ilipunjwa kwenye hesabu za uwekezaji. Hoja ya TTCL inaanzia Novemba 3, 1998 ilipoanzisha kampuni tanzu ya Cellnet ambayo ilifanya kazi mpaka Mei 7, 2001 ilipobadilishwa jina na kuitwa Celtel Tanzania huku umiliki wake ukiendelea kuwa chini ya shirika hilo kwa asilimia zote baada ya kuwekeza Dola milioni tano za Marekani (zaidi ya Sh11 bilioni sasa).Lakini, Januari 31, 2002, Celtel ikiwa chini ya umiliki wa TTCL ilikopa kiasi cha Dola 82 milioni (zaidi ya Sh180.4 bilioni) ili kukuza mtaji wake.Kwa kipindi hicho, TTCL iliyokuwa na thamani ya Dola 600 milioni (zaidi ya Sh1.32 trilioni) ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na Kampuni ya Mobile System International (MSI) ya Uholanzi. Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 65 ya hisa zote na mbia huyo asilimia 35 zilizosalia.Agosti 5, 2005, mabadiliko yalifanywa kwenye bodi ya wakurugenzi wa Celtel kwa lengo la kuunda kampuni mbili tofauti; Celtel ikitenganishwa na TTCL. Kutokana na mabadiliko hayo, Celtel iliwekwa chini ya umiliki wa MSI ambayo Septemba 2007 iliuza hisa zake kwa Zain ambayo nayo ilikuja kuziuza kwa Bharti Airtel, Juni 8, 2010.Imeelezwa kuwa TTCL inadai uwekezaji wake ilioufanya Celtel baadaye Airtel ambayo thamani yake imeongezeka maradufu sasa haulingani na inachokipata hivyo kutaka kusimamia biashara za kampuni hiyo ya mawasiliano.Hoja ya madai hayo ni namna umiliki wa hisa ulivyobadilishwa baada ya Celtel kutenganishwa na TTCL ambayo ilipewa hisa chache tofauti na ilivyostahili.Kwa sasa, Airtel Tanzania inamilikiwa na Serikali yenye asilimia 40 na Celtel Tanzania BV, kampuni tanzu ya Zain Africa BV ambayo ilinunuliwa na Bharti Airtel International, Novemba, 2010 ikiwa na asilimia 60.Katika mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni, Serikali iliilipa Bharti Airtel Sh14.7 bilioni hivyo kuchukua asilimia 35 ya hisa ilizokuwa inamiliki na kuifanya imiliki asilimia zote za TTCL.Sheria mpya iliyopitishwa hivi karibuni na Bunge imeibadili TTCL inayohudumia asilimia 0.82 ya soko kuwa shirika la umma la mawasiliano na kulipa jukumu kubwa katika sekta ya mawasiliano nchini.Bharti Airtel inatakiwa kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ili kukidhi vigezo vya sheria ya posta na mawasiliano ya mwaka 2010, lakini bado haijafanya hivyo.TUME MPYA YAUNDWA KUCHUNGUZA MALI ZA CCM NCHI NZIMA

Taarifa iliyotolewa December 20 2017 kuhusu yaliyojiri katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kikao cha kwanza baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa Tisa wa Mwaka 2017 imeeleza kuwa Rais Magufuli ameunda Tume ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakayokuwa na jukumu la kwenda kufuatilia Mali za Chama kote nchini Tanzania.
Wafuatao wameteuliwa kuwa katika Tume ya CCM ya kufuatilia na kuhakiki Mali za Chama; -
1. Dkt. Bashiru Ali Kakurwa – Mwenyekiti wa Tume
2. Walter Msigwa – Mjumbe
3. Albert Msando – Mjumbe
4. Galala Wabanhu (Hananasif) – Mjumbe
5. Albert Chalamila – Mjumbe
6. William Sarakikya – Mjumbe
7. Komanya Kitwara – Mjumbe
8. Dkt. Fenela Mkangara – Mjumbe
9. Mariam Mungula – Mjumbe
Tume hii itafuatilia mali za Chama kokote ziliko na itamhoji kila mtu anayehusika katika Chama na katika Serikali.

Sunday, July 2, 2017

GEITA KINARA WA MICHEZO

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akimkabidhi kombe mwanafunzi ambaye amewakilisha mkoa wa Geita katika michezo hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba, mkoani Mwanza.

Saturday, July 1, 2017

FATNA RAMOLE MTANGAZAJI WA AZAMN TV HAJULIKANI ALIPO KAMA UMEMUONA POPOTE,SOMA HAPA

 Image may contain: 1 person


Una taarifa zozote kuhusu Fatna Ramole? @fatnaramole
Mfanyakazi mwenzetu @azamtvtz hajulikani alipo.
Unaweza kutoa taarifa zake kwa namba hii
0719669749
Asante. @ Dar es Salaam, Tanzania

MASTAA MBALIMBALI WA SOKA WAHUDHURIA NDOA YA LIONEL MESSI JUNE 30,2017

MESSI AVUNJA UKIMYA ACHUKUA JIKO RASMI
Usiku wa Ijumaa ya June 30 staa wa soka wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi alifunga ndoa na mpenzi wake wa toka utotoni Antonella Roccuzzo ambaye pia wamezaa nae watoto wawili wa kiume.

Messi na Antonella Roccuzzo walifahamiana toka Lionel Messi akiwa na umri wa miaka mitano na Antonella Roccuzzo ambaye ni mke wake kwa sasa akiwa na umri wa miaka 4, wameamua kufunga ndoa kwao Argentina ndoa ambayo ilihudhuriwa na wachezaji wenzake na marafiki zake mbalimbali.
Zaidi ya marafiki wa Lionel Messi wanaofikia 250 walisafiri kwa ndege binafsi kuelekea Argentina kuhudhuria harusi ya staa huyo ambayo simu za mkononi zilikuwa zimefungiwa kufanya kazi ndani ya ukumbi sherehe ilipo kwa lengo la kuweka privacy pamoja na ulinzi wa askari zaidi ya 450.


Rapper wa Marekani, Future amethibitisha show yake ya Tanzania, Julai 22.

TANZANIA YATAJWA KATIKA ZIARA YA MSANII WA MAREKANI FUTUREfuture

Future ametoa orodha ya ziara yake ya muziki ya ‘The Future Hendrxx Tour’ na Tanzania ni moja ya nchi ambayo Tour hiyo itatembelea.
Future atatumbuiza Tanzania pamoja na Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na Weusi.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...