Mtazamo mpya wa Malcolm X juu ya Amerika
Malcolm X anaendelea kusema:-
"Kila
saa ninayopitisha hapa katika Ardhi Takatifu, inaniwezesha kuweza
kuelewa kwa upana zaidi na kupata ufahamu wa kiroho wa yale yanayotokea
Amerika kati ya weupe na weusi. Mnegro wa Amerika asilaumiwe kabisa kwa
uadui wake dhidi ya wazungu weupe. Upinzani anaoufanya (mtu mweusi) ni
matokeo ya miaka mia nne ya ubaguzi wa wazi uliofanywa na Wamarekani
weupe. Lakini wakati ubaguzi wa rangi unaiongoza Amerika katika njia ya
kifo bado naamini, kutokana na uzoefu nilioupata pamoja nao weupe
wazungu, kwamba weupe wa kizazi cha vijana, katika Vyuo Vikuu,
wameshaona ujumbe wa maandishi ulioandikwa ukutani na wengi wao
watageukia njia ya kweli ya kiroho (nayo ni Uislamu); nayo ndiyo njia
pekee iliyobaki kwa Amerika
kuepuka matokeo mabaya ya ubaguzi wa rangi ambao bila shaka ndio utakuwa mwisho wake iwapo hilo halitafanywa.
Ninaamini
kwamba, Mungu anatoa nafasi ya mwisho kwa ulimwengu wa 'Wakristo' weupe
kutubia na kuomba msamaha kwa makosa yao ya kuunyonya na kuutia
utumwani ulimwengu wa wasio weupe. Nayo ni sawa kabisa na wakati
Mwenyezi Mungu alipompa firauni nafasi ya kufanya toba. Lakini Firauni
akadumu katika kukataa kwake kutoa haki kwa wale aliowagandamiza. Na
tunajua Allah mwishowe akamwangamiza Firauni.
Sitaweza
kusahau chakula cha jioni nyumbani kwa Dr. Azzam kwa mwaliko wake
nilipokuwa Jeddah. Jinsi tulivyozidi kuongea, ndivyo hazina yake kubwa
ya elimu ilivyozidi kudhihirika na mambo mengi aliyoyafahamu
yalionekana kama hayana mwisho. Aliongea juu ya kizazi cha Mtume
Muhammad (SAW) na akanifahamisha kwamba walikuwepo weusi na weupe.
Kisha akanielewesha jinsi ambavyo rangi ya mtu na matatizo yake
yaliyopo katika ulimwengu wa Kiislam, yamekuwepo pale ambapo na kwa
kiwango ambacho sehemu ile ya ulimwengu wa Kiislamu imeathiriwa na nchi
za Magharibi. Alisema kwamba kama utakutana na tofauti zozote zenye
msingi wa ubaguzi wa rangi, basi hii moja kwa moja inaashiria kiwango
cha athari zilizoachwa na Umagharib
No comments:
Post a Comment