MUHOGO MCHUNGU ATISHA NA FILAMU MPYA
Muigizaji
mkongwe katika tasnia ya filamu na maigizo ya runingani nchini
Tanazania Abdallah Mkumbilah, ‘Muhogo Mchungu’ anaendeleza makeke
yake ya uigizaji ambapo muda si mrefu anatarajia kutoka katika
filamu zilizobatizwa jina 'Mafia' na 'Dhambi ya Baba'.Katika
filamu hizo Muhogo ameona faraja sana kushirikiana pia na
mwanamasumbwi mahiri nchini ambaye pia ni nyota katika upande wa
ngumi za mateke, maarufu kama Kick Boxing, Japhet Kaseba pamoja na
Kelvin, Mchumia Tumbo na wengineo wengi.
Aidha
kwa upande wa Kaseba ambaye ndiye anasimama kama main character wa
filamu hizo mbili zinazotarajia kuingia sokoni mapema mwakani,
amesema kuwa kushirikiana na gwiji huyo na wengineo wengi kutaleta
msisimko ambapo mara baada ya kumaliza programu za filamu zake hizo
ikiwamo za studio, ataingia tena ulingoni.
No comments:
Post a Comment