Mwaka 1954 mwalimu Julius kambarage nyerere aliporejea
kutoka chuo kikuu cha Edin Burg
uingereza alikutana na viongozi wa chama cha TAA(Tanganyika Africana
Association) wa taifa ndipo alipozungumza nao juu ya kuanzishwa kwa chama cha
siasa,Badala ya chama cha Starehe.
Viongozi hao wa chama cha TAA walikubaliana nae na ndipo
katika mkutano mkuu wa chama cha TAA ,uliofanyika tarehe 7|7|1954 huko mtaa qa
Lumumba kwa sasa,katika ofisi za makao makuu ya TAA,katika mkutano huo ndipo
chama cha TANU kilizaliwa yaani TANGANYIKA AFRICAN NATION UNION) kama chama cha
siasa cha kupigania uhuru wa Tanganyika.
Viongozi haoa walikubaliana kubadilisha chama chao cha
starehe TAA kuwa chama cha siasa cha TANU. Ina maana kuwa matawi Yote ya
majimbo katika nchi ya mikoa 8 ya Tanganyika yaligeuka kuwa matawi ya
TANU,Harakati za kupigania uhuru zikaanza na hata mwalimu nyerere alipita
katika majimbo mbalimbali kueneza chama cha TANU na huko alikutana na viongozi
ambao walimuunga mkono kwa kushirikiana nae katika kupigania uhuru.
Viongozi hao walijitolea
kupokea na kumkaribisha Mwalimu hata kumpatia usafiri,malazi na chakula.
Ifahamike wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao wa matawi walitoa michango
mbalimbali na wapo waliopata matatizo mbalimbali katika kupigania uhuru huo
kama vile wapo waliopoteza mali zao,waliofungwa na hata waiotengwa na familia
zao na jamii pia.
Vilevile mwalimu ilibidi aache kazi na waliamua ahamie
Magomenim mjini dar es salaam katika nyumba ya kupanga,mwalimu alipata
misukosuko kama vile kushtakiwa mahakamani lakini pamoja na misukosuko
hiyo alifanikiwa kwenda New york
Marekani katika baraza kuu la umoja wa mataifa(UNO) na kuwasilisha hoja za
Tanganyika kupata uhuru,lakini ililazimika kufanyike uchaguzi wa kura tatu.
Kura tatu ni uchaguzi ambao kila chama cha siasa ilibidi
kuweka wagombea watatu Mzungu,Mwasia na Mwafrika, uchaguzi ambao chama cha TANU
kilifanikiwa kupata ushindi.
Hatimae mwaka 1960
tulipata serikali ya madaraka ya ndani, 1961 tukapata uhuru na 1962 tukapata
Jamhuri. Inabidi ifahamikeni kina nani wameshiriki katika kupigania uhuru wa
nchi yetu,inabidi jamii ya Tanzania ijue ni kina nani wameshiriki kikamilifu
katika kupigania uhuru wan chi yetu katika ngazi ya taifa.
Mbali na hayo tujue ni wazee gani kwa majina wameshiriki kupigania
uhuru katika ngazi ya mkoa,wilaya hata majimbo. Katika harakati za kupigania
uhuru wapo waliopata matatizo mengi kama vile wapo waliopoteza mali,ajira na
hata ndoa zao kuvunjika, kufungwa magerezani na wengine kutengwa na jamii kwa
sababu ya kupigania uhuru .
Lakini leo hakuna mtu yeyote katika wasomi wetu wa
historia,Viongozi wa juu,wanasiasa na jamii ya watanzania kwa ujumla
inaowakumbuka au kuwataja,kwanini kusifanyike utafiti wa kina utakaowezesha
kutambuliwa kwa watu hao na hata ikiwezekana serikali ya sasa kuwalipa fidia
kwa Madhara waliyoyapata kutokana na kutetea na kupigania uhuru wa nchi hii kwa
kuwapa nishani,kwa kufanya hivi itakuwa halali kuwa waliopigania uhuru wa nchi
hii mchango wao umetambulika na wamefahamika kwa watanzania.
Je ni uongo hakuna wazee wanaolalamika kuwa walishiriki
kupigania uhuru wan chi hii ya TANZANIA kwa sasa lakini wanajutia mchango wao
huo kwa sasa kwani Viongozi walipokwisha pata uhuru wao na kufaidi matunda ya
uhuru,sasa wao wamekuwa hawana maana
tena, JE NI HALALI KUTOWAKUMBUKA?
Kwa mfano mdogo ukimuuliza mwanafunzi aliyemaliza kidato cha
nne ni majina ya watu gani yaliyoanzisha
chama cha TANU? Mzee Derick Bryson alikuwa nani? Hata mzee Rashid kawawa
hawajui mchango wake katika kupigania uhuru w a nchi hii
Je kutofahimika kwa wapigania uhuru wa kitaifa,mkoa ,wilaya
na je kuna sababu zipi za kutoandika historia ya kweli ya harakati za kupigania
uhuru baada ya miaka 50,iwe tunamtaja Mwalimu nyerere peke yake?
Kwa maoni yangu nafikiri ingekuwa bora sana tunapozungumzia Nyerere Day basi ni
vyema wakakumbukwa na wapigania uhuru wengine kwa kuwataja majina yao kwa
kuthamini mchango wao wa kupigania uhuru ambao leo hii sisi ndio tunaokula
matunda yake.
IMEANDALIWA NA MMILIKI WA BLOG
Email: Stambulin1991@gmail.com,
No comments:
Post a Comment