airtel

airtel

.

.

Monday, February 25, 2013

KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA MILOVAN CIRKOVIC AMELIPWA PESA ZAKE ZOTE DOLA 32,000 ALIZOKUWA AKIIDAI CLUB YA SIMBA


Kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic.
KOCHA wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic, amesema amepokea fedha zake dola 32,000 (Sh milioni 51.2) na nyongeza ya dola 3,000.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Milovan, raia wa Serbia, alisema amepokea fedha hizo baada ya mkewe kumtaarifu kila kitu safi.
“Mke wangu amekwenda benki, ameangalia na kaniambia tayari fedha nilizolipwa na Malkia wa Nyuki zimeshaingia katika akaunti yangu. Nashukuru sana kwa uungwana aliouonyesha huyu mama.
“Nilijaribu kumtafuta kwa ajili ya kumshukuru lakini sikufanikiwa, tayari kuna watu nimezungumza nao wanifikishie shukurani zangu kutokana na kunilipa haki yangu na kuonyesha uungwana wa hali ya juu,” alisema Milovan.
“Nafikiri nitaondoka ndani ya siku mbili, ila nitaangalia mechi ya mwisho ya Simba leo (jana), halafu nitawaaga wachezaji na rafiki zangu kama nitapata nafasi na baada ya hapo nitafanya utaratibu wa kuondoka kurejea nyumbani.”
Rahma Al Kharusi ndiye alijitokeza na kuamua kumlipa Milovan fedha hizo ambazo ni mishahara ya miezi minne, mitatu kati ya hiyo ni kwa ajili ya kuvunja mkataba.
Tangu alipotua nchini, viongozi wa Simba wamekuwa wakimkimbia hata wale waliokuwa marafiki zake. Lakini tangu alipwe, angalau baadhi wamekuwa wakizungumza naye na kurejesha urafiki wao wa zamani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...