Muasisi wa kundi maarufu wa muziki wa Bongo Flava aitwaye BARAKA MARTIN
SEKELA aka BK , amefariki alfajili ya leo katika Hospitali ya Muhimbili
ambako alikuwa amelazwa , kwa mujibu wa Hassan Isaack Umande ambaye
amewahi kuwa meneja wa kundi hilo, mwili wa marehemu bado upo
hospitalini hapo na familia ya marehemu inajipanga kwa mazishi. Baadhi
ya Nyimbo aliwahi kuchana ni Ndege Tunduni (verse
ya kwanza), Tatu Bila, kabla ya hizo ni Sitaki Dem Rmx ya Juma Nature,
Kwa Maisha alioshirikishwa na Temba na ktk traki kali inayoitwa
Tunavyoishi wakiwa na Suma Lee na Dollo.Pia marehemu amewahi kurekodi
traki zake mwenyewe , bado najipanga baadaye nitaeleza zaidi kwani mimi
King Kif nimewahi kufanya naye shughuli nyingi za muziki.
kwenye hii picha kushoto ni mshabiki wa kundi hilo, katikati ni marehemu
BK halafu Dotto aka D Chief .Mwenyezi Mungu mlaze mahali pema peponi
marehemu BKna mchango wako utakumbukwa daima kwenye gemu la Bongo.Amina |
|
|
|
No comments:
Post a Comment