airtel

airtel

.

.

Monday, February 25, 2013

RAISI JAKAYA KIKWETE AMESHIRIKI MAZISHI YA KUMZIKA MZEE AMOS KAGUTA KATIKA KIJIJI CHA RWAKITURA NCHINI UGANDA,PAMOJA NA KUTOA POLE KWA FAMILIA YA RAISI WA UGANDA

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua juu ya jeneza la Marehemu Mzee Amos Kaguta(97),Baba Mzazi wa Rais Wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijiji Cha Rwakitura nchini Uganda.
 
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiweka udongo kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta(97) wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura.
   Rais Dkt.Jakaya Kikwete akimpa pole Rais Yoweri Kaguta Museveni kutokana na kifo cha Baba yake Mzee Amos Kaguta, katika kijiji cha Rwakitura nchini humo.
 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akifariji mke wa Rais wa Uganda Mama Janet Museveni kufuatia kifo cha Baba wa Rais Museveni Mzee Amos Kaguta.Picha na Freddy Maro-IKULU

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...