Kwa wale wapenzi wa movies za hollywood na mashabiki wa Angelina Jolie kuna habari yake nzito.
Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.
Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New
York Times, Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na
kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani
ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama na watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.
Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa
uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na
asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.
''Niliamua kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,'' alisema Jolie.
Alisema kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi April.
Katika taarifa iliyoandikwa Jolie na yenye
kichwa, 'Uamuzi wangu wa kimatibabu',Jolie alieleza kuwa mamake
alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki akiwa na umri wa miaka
56.
Alisema kuwa alielewa fika kuwa siku moja
atawahi kuugua Saratani na ndio maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa
upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti.
Uwezekano wake wa kuugua saratani sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%.
Alimsifu mumewe Brad Pitt, kwa kumuunga mkono na
kumfariji kwa kila aliyopitia, na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanawe
hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu
kufanyiwa upasuaji.
"ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi niliofanya,
na kwa kuwa ninasalia kuwa mwanamke hata baada ya kuondoa viungo
hivyo,'' alisema Bi Jolie.
"kwa mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza kufanya uamuzi.''
Muigizaji huyo, ambaye ameshinda tuzo nyingi kwa
uigizaji wake, pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalum wa Umoja wa
Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.
Wakati alipokuwa anafanyiwa upasuaji, Bi Jolie
alizuru Jamuhuri ya Kidremokrasia ya Congo pamoja na waziri wa mambo ya
nje wa Uingereza William Hague.
Jolie pia alihudhuria mkutano wa mawaziri wa
mambo ya nchi za kigeni wa G8, kuhamasisha dunia kuhusu dhulma za
kingono katika maeneo yav ita.
Angelina Jolie pichani na mumewe na watoto.
No comments:
Post a Comment