Rais
wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 01 Julai,
2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.
Katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais
Obama ambaye atafuatana na Mkewe Mama Michelle atapokelewa na Mwenyeji wake,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Baada
ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete.
Aidha, atafanya mkutano na Wafanyabiashara na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.
Tarehe
2 Julai 2013, Mhe. Rais Obama atatembelea Mitambo ya kufua Umeme ya Symbion
iliyopo Ubungo, Dar es Salaam na kuzindua rasmi Mpango Maalum wa Maendeleo ya
Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na Marekani (Power Africa Initiative).
Mpango
huo utaanza na nchi saba ambazo ni: - Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Ghana,
Nigeria na Sudan Kusini.
Mhe.
Rais Obama anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 02 Julai 2013.
IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA
NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
30 JUNI, 2013
No comments:
Post a Comment