Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto (kulia) aktinga rasmi ofisi za Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto(Kushoto)akiteta jambo na wakili
wake, Albert Msando wakitoka Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu (kushoto) na Wakili wa chama
hicho, Peter Kibatala (katikati) wakitoka katika chumba cha Mahakama Kuu
jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto(Kulia)akifurahia jambo na wakili
wake, Albert Msando wakitoka Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto(Kushoto) na wakili wake, Albert Msando wakitoka Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Zitto Kabwe jana alitinga mahakama kuu kupinga kujadiliwa
kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao ambacho kilikuwa kikutane
leo.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu(Kushoto)akiteta jambo na Mbunge wa Arusha Mjini -Godbless Lema.Picha na Fidelis Felix
-----
Mahakama Kuu Tanzania, imeizuia kwa muda Kamati Kuu ya Chadema
kujadili ajenda zozote zinazomhusu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake,
Zitto Kabwe hadi ombi lake la rufaa litakaposikilizwa.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji John Utamwa
baada ya kupokea maombi ya Zitto kupitia kwa Wakili wake, Albert Msando
kutaka rufaa yake aliyoiwasilisha Baraza Kuu kusikilizwa kwanza kabla ya
kufanyika uamuzi mwingine.
Kamati Kuu ya chama hicho, ilipanga kukutana leo
ikiwa na ajenda kuu tatu; kupanga mpangokazi wa chama kwa mwaka 2014,
kupokea utetezi wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali
zilizoelekezwa kwao na kupokea taarifa kuhusu mchakato wa mabadiliko ya
Katiba.
Zuio la Mahakama
Zuio hilo lilikuja pia baada ya kutupiliwa mbali
maombi ya pingamizi la Chadema lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Katiba
na Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Peter Kibatala.
Akizungumza jana baada ya uamuzi huo wa Mahakama, Mwanasheria Mkuu Chadema, Tundu Lissu alisema hakuna jinsi zaidi ya kukubaliana na uamuzi huo... “Tumekubali kutokumjadili Zitto lakini tuliomba Mahakama iruhusu kuhojiwa kwa Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
No comments:
Post a Comment