Wajumbe wa bunge la Katiba mpya wamepitisha kura ya wazi na siri
kutumika kwa pamoja katika kuendesha bunge hilo la katiba baada ya
majuma kadhaa ya mabishano juu ya utaratibu upi utumike.
Tangu
kuanza kwa bunge maalum la katiba kwa zaidi ya siku 40 mgongano mkubwa
umekuwa katika kanuni za 37 na 38 kuhusu suala la upigaji wa kura za
wazi na siri.
Makubaliano ya kura
ya wazi na siri yanaanzia katika upigaji kura wa kuridhia mapendekezo
hayo ya kanuni waliotaka kura za siri haya,wa kura za wazi na sawa.
Tayari wajumbe hawa wametumia siku 40 kutunga na kupitisha kanuni za
kuweza kusimamia shughuli za uendeshaji wa bunge hili maalum la katiba
mjini Dodoma.
Chini ya kamati ya muda ya maridhiano baada ya
kukaa kwa masaa kadhaa tangu usiku wa machi 27 kimsingi wamekubaliana
kuendelea na mchakato wa utungaji wa katiba mpya.
Mwisho
No comments:
Post a Comment