Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian
Lubuva akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam jana.
Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Julius Mallaba.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifanya kazi yao kwa umakini wakati Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo
pichani) wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu
ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.
Baaadhi
ya wakuu wa Idara toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza kwa
makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian
Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati
akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya
uandikishaji wapiga kura nchini.
Baadhi
ya wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo
jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya
habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.
Baadhi ya wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Baadhi
ya wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo
jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya
habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini. Picha zote na Eliphace Marwa – MAELEZO
---
Na: Frank Shija, Maelezo
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarijia kuanza zoezi la Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mapema mwezi Septemba 2014, ikiwa ni
maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na upikaji wa Kura za
Maoni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa
Tume hiyo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Damian Lubuva wakati
akifungua Mkutano wa NEC na Wahariri wa Vyombo vya Habari, leo jijini
Dar es Salaam.
Jaji Lubuva amebainisha kuwa
uborehasji wa Daftari la Wapiga kura litatumia mfumo mpya wa
Kiteknolojia ujulikanao kama Biometric Voter Registration (BVR) ambapo
katika mfumo huo taarifa za mtu za Kibiolojia au tabia ya mwanadamu
zitachukuliwa na kuifadhiwa kwenye kanzi data ya Wapiga Kura.
Katika mfumo huo wananchi wote
wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na Kadi za Mpiga Kura
watatakiwa kuandikishwa upya ili kupata Daftari sahihi linaloaminika
zaidi kwa ajili ya upigaji Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Uamuzi wa kutumia mfumo huo mpya wa
kuandikisha wapiga kura umefikiwa baada ya kubaini kasoro mbalimbali
zilizokuwepo kutokana nma kutumia mfumo wa zamani wa Optical Mark
Recognition (OMR) hadi kupelekea baadhi ya wadau wa uchaguzi kupigia
kelele mfumo huo,
Aliongeza kuwa kutumiika kwa mfumo
wa BRV kutasaidi kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye Daftari
lililopo ikiwemo kuzuia mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja.
“Ndugu zangu wahariri ni ukweli
ulio dhahiri kwamba matumizi ya OMR yalisababisha kwa kiasi kikubwa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuwa na kasoro,zilizopelekea baadhi ya
wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake. Hivyo ni mategemeo ya Tume ya
Taifa ya Uchaguzi kuwa matumizi ya BVR yatapunguza au kuondoa kabisa
matatizo yaliyomo kwenye Daftari lililopo”. Alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva alitumia nafasi
hiyo kutoa rai kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kutoa ushirikiano kwa
NEC ilikufanikisha zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura
kwa kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi ili waapate uekewa wa
mfumo huu mpya utakaomtumika katika zoezi hilo, na kutoa hamasa
wajitokeze katika viotuo vya kujiandikishia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Uchaguzi Julius Malaba amesema kuwa maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa
Daftari la Wapiga Kura umekamilika kwa asilimia kubwa ikiwa ni pamoja
na kufanya uhakiki wa vituo vya kujiandikishia ambapo jumla ya vituo
40,015 vimeainishwa kutoka vituo 24,919 vilivyokuwepo awali.
Malaba aliongeza kuwa ongezeko hilo
la vituo limetokana na kushusha zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura
kutoka ngazi ya Kata, na sasa utafanyika kuanzia ngazi ya
Vitongoj,Vijijii na Mitaa ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wananchi.
Malaba aliongeza kuwa Tume
inatarijia kupokea vifaa kwa ajili ya zoezi hilo mapema mwezi Aguosti
2014 kwa aijili ya kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga
Kura, na kuongeza kuwa vifaa vichache vitawasili mapema mwezi julai
kufanikisha mafunzo kwa watendaji watakao husika na zoezi la Uboreshaji
wa Daftari la Mpiga Kura.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Mpiga Kura linatarijiwa kuanza mwezi septemba 2014 ambapo kila kituo cha
kujiandikisha kinakadiriwa kutumia siku 14 hadi zoezi kukamilika , na
jumla ya takribani shilingi Bilioni 293 zinatarajiwa kutumika katika
zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment