France imefanikiwa kuingia Robo Fainali ya Kombe la Dunia huko Brazil baada ya hii Leo kuitwanga Nigeria Bao 2-0.
Bao zote za Mechi hii zilifungwa Kipindi
cha Pili na la kwanza kwenye Dakika ya 79 kwa Kichwa cha Paul Pogba
baada ya Kipa Enyeama kushindwa kuicheza Krosi na kumkuta Pogba
aliemalizia kilaini.
Bao la Pili lilifungwa Dakika ya 91 na
ni la kujifunga mwenyewe Joseph Yobo baada ya Krosi ya chini ya Mathieu
Valbuena kuchinjwa na Antoine Griezmann na Mpira kumgusa Yobo na kutinga
wavuni.
Kwenye Robo Fainali, France itacheza na Mshindi kati ya Germany na Algeria wanaocheza baadae Leo hii.
VIKOSI:
NIGERIA: Enyeama, Ambrose, Yobo, Oshaniwa, Omeruo, Onazi, Mikel, Musa, Odemwingie, Moses, Emenike.
Akiba: Ejide, Agbim, Uzoenyi, Gabriel, Egwuekwe, Odunlami, Oboabona, Azeez, Nwofor, Uchebo, Ameobi.
FRANCE: Lloris, Debuchy, Evra, Koscielny, Varane, Cabaye, Valbuena, Benzema, Matuidi, Pogba, Giroud.
Akiba: Ruffier, Landreau, Sakho, Cabella, Griezmann, Mavuba, Mangala, Sagna, Digne, Sissoko, Remy, Schneiderlin.
Refa: Mark Geiger (USA)
No comments:
Post a Comment