Taarifa iliyotolewa December 20 2017 kuhusu yaliyojiri katika Kikao
Cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kikao cha kwanza baada ya Mkutano
Mkuu wa Taifa wa Tisa wa Mwaka 2017 imeeleza kuwa Rais Magufuli ameunda
Tume ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakayokuwa na jukumu la kwenda
kufuatilia Mali za Chama kote nchini Tanzania.
Wafuatao wameteuliwa kuwa katika Tume ya CCM ya kufuatilia na kuhakiki Mali za Chama; -
1. Dkt. Bashiru Ali Kakurwa – Mwenyekiti wa Tume
2. Walter Msigwa – Mjumbe
3. Albert Msando – Mjumbe
4. Galala Wabanhu (Hananasif) – Mjumbe
5. Albert Chalamila – Mjumbe
6. William Sarakikya – Mjumbe
7. Komanya Kitwara – Mjumbe
8. Dkt. Fenela Mkangara – Mjumbe
9. Mariam Mungula – Mjumbe
Tume hii itafuatilia mali za Chama kokote ziliko na itamhoji kila mtu anayehusika katika Chama na katika Serikali.
No comments:
Post a Comment