DONDOO MUHIMU KATIKA MAJUMUISHO
- Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Simbakalia kawaomba radhi wananchi wa Mtwara.
- Waziri Nchimbi ameahidi suala la usalama ni la kila mmoja,amani na utulivu vinahitajika katika kujenga demokrasia ya kweli,pia jeshi lake litakuwa karibu na raia
- Kawambwa kawahimiza wazazi kuwaruhusu watoto kwenda shule kupata elimu sanjari na chuo cha VETA kutoa masomo ya mitaala ya gesi sanjari na uchomeleaji baharini.
- Tibaijuka amezungumzia kuhusu upanuzi wa mji wa Mtwara na kuleata kauli mbiu ya "Amani na maendeleo" kutoka kwao Kagera.
- Mwakyembe amezungumzia upanuzi wa bandari kavu na ujenzi wa reli Mtwara, Liganga, Mchuchuma hadi Mbamba bay na kuahidi kuja Mtwara kila baada ya miezi 3 na kujadili na kutathmini changamoto.
- Waziri Mkuu ametoa udhuru wa waziri wa ujenzi Dr Magufuli ambaye alitakiwa kuwepo lakini hataweza kuhudhuria.
- Bi Mapunjo kaahidi mipango mikubwa ya ujenzi wa viwanda mkoani Mtwara.
- Mbilinyi kaainisha idadi ya makampuni yaliyoonyesha nia ya kuja kuwekeza Mtwara
- Waziri Mkuu katoa majumuisho ya ziara yake ambayo hayana tofauti na haya yaliyojadiliwa.
- Nasta boy blogspot.com inaipongeza serikali kwa hatua hii ya kutafuta muafaka wa suala la gesi na ni matumaini kuwa wana mtwara watanufaika na rasimali hii muhimu.
No comments:
Post a Comment