airtel

airtel

.

.

Thursday, January 17, 2013

PROFESSOR JAY: NIMEKUBALI UJIO MPYA WA VANESSA MDEE

       Mapema leo hii, Joseph Haule a.k.a Profesa Jay alikitambua na kukisifia kipaji cha mwanamuziki mpya na mtangazaji Vanessa Mdee na kumshauri akitilie mkazo. Vanessa ambae ameachia bonge ya ngoma inayofahamika kama #CLOSER ambayo inafanya vizuri sana wakati huu, alipewa ushauri huo na Profesa Jay kwa kuangalia upande wa pili kuwa ameweka kwenye kupenda tu anachofanya (hobby) katika muziki na sio SERIOUS kama anavyoonekana.

       Profesa Jay alionekana kufurahia kipaji kipya hiki na kuandika katika ukurasa wake wa twitter na kukitaka kitilie mkazo ili kujaribu kuonesha utofauti kwenye game ya muziki huu wa Tanzania na kuufikisha mbali.
Vanessa alijibu na kusema ahsante na kwamba atalifanyia kazi hili. Vanessa Mdee alirekodi track kadhaa alizofanya kama collabo kabla lakini weekend iliyoisha aliachia wimbo wake mpya unaojulikana kama CLOSER na kuonesha ni jinsi gani anaweza.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...