airtel

airtel

.

.

Friday, February 1, 2013

GARI LA MAREHEMU SHARO MILIONEA LAUZWA NA MAMA YAKE MZAZI


.
Gari aina ya Toyota Opa aliyoiacha marehemu Sharo Milionea.
MAMA wa aliyekuwa msanii wa muziki na filamu Bongo, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefungukia gari aliloacha mwanaye pamoja na mimba ambayo inadaiwa ni yake
 Mama Sharo ameongea na nastaboy blogspot kuthibitisha na hapa namnukuu: “Kuhusu gari lile Toyota Opa aliloacha marehemu mwanangu naliuza kwani siwezi kuliendesha na haliwezi kukaa bila kufanya kazi yoyote.
“Kwa upande wa Marry Lucas wa Sumbawanga msichana aliyejitokeza baada ya Sharo kufariki na kusema ana ujauzito wake, siwezi kumtambua kwa sababu enzi za uhai Sharo hakuniambia kuwa ana mchumba wala mpenzi.”
Sharo Milionea alifariki dunia Nov 26, mwaka jana kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Tanga.
Siku chache baadaye, Marry aliibuka na kudai alikuwa mpenzi wa Sharo na ana ujauzito wake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...