Waziri wa elimu wa Ujerumani,
Annette Schavan, amevuliwa cheo chake cha Daktari wa Falsafa, baada ya
kugundulika kuwepo na wizi wa mawazo ya mtu.
Chuo Kikuu cha Düsseldorf
kilichoko mashariki wa Ujerumani, kimesema jana jioni kuwa Schavan
hakuonyesha vyanzo ipasavyo katika shahada yake ya juu ya mwaka 1980,
ambayo ilichunguza uundwaji wa dhamira na kwamba kwa maksudi alichukuwa
mawazo na kuyaonyesha kama ya kwake.
Madai kuwa Schavan aliiba
mawazo ya sehemu ya shahada yake ya juu, yalianza mwaka uliyopita,
wakati madai yasiyo na jina yalipochapishwa kwenye mtandao wa intaneti.
Schavan siyo mwanasiasa wa
kwanza maarufu nchini Ujerumani kudaiwa kuiba mawazo mwaka 2011,
aliyekuwa waziri wa ulinzi Karl-Theodor zu Guttenberg alivuliwa shahada
yake ya juu na kulaazimishwa kujiuzulu.
No comments:
Post a Comment