
Kaimu
Mkurugenzi Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Mary Meela
akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Mikakati wanayoweka ya
kuendelea kudhibiti ubora wa bidhaa nchini ikiwemo kuimarisha ukaguzi kwenye
vituo vya mipakani mwa nchi,Kulia ni Afisa Habari Wa Idara ya Habari Bw.
Frank Mvungi.
|

Afisa
Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile akitoa wito
kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuendelea kuelemisha umma kuhusu
madhara ya matumizi ya nguo za mdani za mtumba. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Udhibiti Ubora wa Shirika hilo Bi. Mary Meela.Picha na Hassan Silayo
---
Na Frank Mvungi
Shirika la viwango Tanzania (TBS) linatarajia kuajiri watumishi
200 katika harakati za kuimarisha utendaji wa shirika hilo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa udhibiti ubora wa shirika
hilo Bi Mary Meela wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam.
Akifafanua Meela amesema watumishi watakaoajiriwa watasaidia
kuimarisha utendaji kazi wa shirika hilo hasa katika kufanya ukaguzi na
kuhakisha tatizo la bidhaa hafifu linapungua au kuondolewa kabisa.
Aidha Bi. Meela alisema kuwa Shirika limeweza kuweka wakaguzi
kwenye vituo 5 ambavyo ni Sirari, Namanga, Taveta, Horohoro, Bandari za Tanga
na Dar es salaam na kuweka wakaguzi kwenye vituo vya bandari kavu (ICD).
Akizungumzia kuhusu utumiaji wa nguo za ndani za Mtumba Bi. Meela
amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya nguo hizo kwani
zina madhara kiafya kwa watumiaji na wataendelea kufanya ukaguzi wa nguo hizo
na kuziteketeza pindi zinapopatikana.
Shirika la viwango lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 3 ya mwaka
1975, kasha kuundwa upya mwaka 2009 sheria ambayo imelipa shirika uwezo mkubwa
zaidi wa utayarishaji viwango na kusimamia utekelezaji wake
No comments:
Post a Comment