airtel

airtel

.

.

Sunday, January 4, 2015

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUAPISHWA JUMATATU

Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, George Mcheche Masaju.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa Kesho Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...