airtel

airtel

.

.

Monday, August 3, 2015

MH.NUNDU AIBUKA KIDEDEA KATIKA KURA ZA MAONI ZA CCM JIJI LA TANGA



 
Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Omar R.Nundu (pichani), ambaye kwa sasa amehamia  ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama chake MAPINDUZI MKOA WA TANGA.
 
NUNDU aliibuka mshindi kati ya wagombea Sita kwa kupata kura 7557 kati ya 20796 zilizopigwa.
na wanachama wa ccm mkoa wa tanga.
 
 kura zilizotarajiwa kupigwa zilikuwa ni 51,003, lakini zilipigwa 20,796 na wagombea wengine wa nafasi hiyo na idadi ya kura zao walizopata kwenye mabano ni kisauji (7004), kassim mbughuni (1801) , kassim makubeli (1728),Athumani hassan (1448) na meja mstaafu Hamisi B. mkoba (1258)
 
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, NUNDU alisema ushindi huo ni wa wanatanga wote na wanachama wa chama cha mapinduzi na kuhimiza ushirikiano kuelekea ushindi katika uchaguzi mkuu oktoba 25.
Pamoja na matokeo hayo Wakazi wa Tanga wamekubaliana na matokeo hayo huku wakilaumu wakusanyaji wa matokeo hayo kuchelewesha kutangaza matokeo hayo hali iliyozua sintofahamu kwa wanachama na wakazi wa jijini hapa ambao walishtushwa na vichwa vya habari za magazeti ya jumapili yalikuwa na habari Nundu aanguka.
blog hii inatoa pongezi za dhati kwa Mbunge nundu kwa ushindi na kumtakia kila la kheri katika maandalizi ya kampeni zinazotarajia kuanza agosti 22.
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...