Kassu Ent iliandaa
tamasha maalum kutoka kwa wasanii wetu wa kizazi kipya iliowajumuisha
Barbaba na Suma Lee. Tamasha hili lilikwenda sambamba kwa kusherekea
miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika siku ya jumamosi tarehe
22.12.12 jijini London katika ukumbi wa Stratford.
Mgeni rasmi alikua
naibu Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na mkewe Irene Kilumanga.
Aidha Mh Balozi Kilumanga aliwapongeza watanzania walioweza kuja
kujumuika na kusherekea pamoja katika siku hii na kuwasihi kuendeleza
mshikamano kwa kuishi pamoja kwa amani na upendo.
Kwa maelezo zaidi picha na tarehe za shoo zijazo tembelea www.jestina-george. com
Taarifa imetumwa na Frank Eyembe wa Urban Pulse.
No comments:
Post a Comment