airtel

airtel

.

.

Monday, December 17, 2012

NDEGE YA TANAPA YAANGUKA JIONI HII MKOA WA KATAVI



0
.
.
.
.
Ndege ya shirika la hifadhi la taifa (TANAPA) aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa alieumia sehemu ya uso.
Ajali imetokea jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi ambapo meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda  Mahamud Muhamed  kasema ajali ilitokea jana december 16 2012 saa kumi na dakika 55 jioni.
Ni ndege ya abiria mali ya hifadhi ya taifa ya  TANAPA na una uwezo wa kuchukua abiria wanne na imeanguka umbali wa kilometa moja na nusu kutoka uwanja wa ndege.
Meneja wa uwanja  huo wa ndege  alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo  cha ajali ni injini ya ndege kufeli wakati ikiwa angani.
Rubani wa ndege hiyo alipata msaada kutoka kwa wananchi waliokuwa  shambani mwao ambapo mmoja wao alisema wakati akiwa anafanya shughuli  zake  za kilimo ghafla aliona ndege angani  ikizimika injini na muda mfupi baadae ikaanguka jirani na mti wa mwembe, kazi ya uokoaji ilichukua muda kidogo kutokana na nyuki.
(Taarifa imeandikwa na http://kataviyetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...