Rais Kikwete akagua Ukumbi Mpya Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi mkubwa
wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert
jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika
hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo
ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha
na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais
Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili
kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali.
No comments:
Post a Comment