Msanii timbulo akiwa chini ya ulinzi wa polisi |
hizi ndio kete alizokamatwa nazo huko bujumbura |
Msanii wa Bongo flava maarufu kwa jina la Timbulo, ambaye amepata umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wa kuimba katika nyimbo zake kadhaa kama Domo Langu, Waleo Wakesho, Samson na Delilah,amekana tuhuma za kukamatwa mjini Bujumbura kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya. Timbulo alikuwa huko katika kufanya mipango ya kufanya maonyesho kadhaa nchini Burundi mwezi April mwaka huu.
Hata hivyo blog hii ilifanya jitihada ya kumtafuta meneja wa timbulo ambae alisema kuwa picha zilizotumiwa na baadhi ya vyombo vya habari kumchafua msanii huyo ni moja ya scene zilizopo katika filamu mpya itakayotoka ambayo timbulo ameigiza,na hivyo kuwatoa hofu mashabiki wa msanii huyo.
No comments:
Post a Comment