Uongozi
wa shirika la reli TRC Dodoma umeagizwa kuwagharamia abiria wake
waliokwama station ya Dodoma huduma za chakula na nyingine muhimu kwa
kipindi chote watakaposubiria kukamilika kwa matengenezo ya njia ya reli
eneo la godegode mpwapwa na hatimae abbiria hao kuendelea na safari yao
kuelekea Dar es salaam.
Kwa
mujibu wa abiria hao waliokwama station ya Dodoma wameelezea kuwa
walikata tiketi ili kuondoka Kigoma januari 2 lakini walikwama mpaka
Jumanne januari 7 sababu kubwa ikiwa ni kupata hitilafu kwa treni ya
mizigo kwenye njia ya reli hivyo na hatimae kufika Dodoma Januari 9
asubuhi ambapo uongozi wa TRC Dodoma uliwafahamisha kuwa kuna tatizo la
kuharibika kwa njia ya reli eneo la Godegode, Mpwapwa, hivyo watasubiri
mpaka jioni ya leo ndipo waendelee na safari ya Dar es salaam.
Hayo
yalibainika leo wakati abiria hao waliokwama walipoandamana hadi ofisini
kwa mkuu wa mkoa Dodoma kuonana naye na kuelezea adha wanayopata baada
ya kukwama kwa safari yao ikiwa ni pamoja na kuingia gharama kubwa ya
chakula, huduma nyingine muhimu kwenye vituo walipokwama na wengine
wanawatoto na wagonjwa na hadi sasa wameishiwa kabisa fedha.
Kwa
mujibu wa mkuu huyo wa mkoa dodoma, amewaagiza TRC Dodoma kuwagharamia
chakula na huduma hizo muhimu mpaka watakapoendelea na safari yao
kuelekea Dar es salaam.
Aidha
Dr. Nchimbi ameelezea kuwa eneo hilo la Godegode lina tabia ya
kutiririsha mikondo mikubwa na yenye nguvu ya maji yanayokusanyika
kutoka milimani na hata meneo ya mikoa ya jirani kama.
Kwa
upande wake mhandisi mitambo wa TRC Dodoma bw. John Mandalu amesema kazi
ya marekebisho ya eneo la Godegode lililoharibika inaendelea vizuri, na
itakamilika jioni ya leo na safari itaendelea na kuwa kwa muda wote wa
kusubiri huduma kurejea TRC itagharamia huduma za chakula na nyingine
muhimu.
Taarifa
zilizopatikana ofisi ya mkuu wa wilaya ya Dodoma zinasema kuwa hadi
kufikia jioni ya Leo matengenezo ya njia ya njia ya reli yalikuwa
yameshakamilika na safari itaendelea kama ilivyopangwa kuendelea jioni
Abiria
waliokwama Mkoani Kigoma tangu januari 2 na hatimaye leo kufika Dodoma
na kukwama tena baada ya kuharibika kwa njia ya reli eneo la Godegode
mpwapwa wakichaguana wawakilishi wao wa kwenda kuzungumza na mkuu wa
Mkoa Dodoma kumweleza adha wanayopata asubuhi ya leo walipokwenda
ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa kwa maandamano, pembeni ni askari wa
kulinda ulinzi na usalama.
Wasafiri
wawakilishi wa treni ya kati waliokwama station ya dodoma wakipeana
mrejesho na wenzao juu ya kile walicho kubaliana na mkuu wa Mkoa Dodoma
mara baada ya kumaliza kuzungumza naye.
Mkuu
wa Mkoani dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na abiria wa treni ya
kati waliokwama Mkoani Kigoma tangu januari 2, na kukwama tena Leo
Mkoani dodoma mara baada ya kuwasili Mkoani humu kufuatia uharibifu wa
njia ya reli, vilevile mkuu huyo wa mkoa amewaagiza uongozi wa shirka la
reli mkoani Dodoma kuwagharamia kwa huduma ya chakula na nyingine
muhimu mpaka watakapoendelea na kumalizia safari yao.
Wawakilishi
wa abiria wa treni waliokwama mkoani dodoma (watatu walioko kulia)
walioteuliwa kwenda kuonana na mkuu wa mkoa wa dodoma kuelezea adha
wanayopata baada ya kukwama kwa safari yao wakisikiliza maelekezo ya
mkuu wa Mkoa wa dodoma (hayupo pichani) mapema leo, wengine kushoto ni
maafisa wa jeshi la polisi Dodoma.
No comments:
Post a Comment