airtel

airtel

.

.

Thursday, January 9, 2014

TAZAMA PICHA KUMI ZA UZINDUZI WA TAASISI YA MWAHARAKATI BIBI SITI BINTI SAAD


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(kushoto) akiwa mlezi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad akifuatiwa na Mwenyekiti wake Bibi Nasra Mohamed Halal, wengine kulia Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk,wakiwa katika Uzinduzi wa Taasisi hiyo iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hote, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Prof Laura Fair, aliyefanya utafiti na kutunga kitabu cha wa mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,akizindua kitabu hicho wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya mwanaharakati huyo iliofanya jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shei,(hayupopichani) katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel mjini Unguja,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Historia ya Harakati za wanawake iliyotolewa na Dk.Amina Ameir,mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na kumpongeza Dk.Amina Ameir,baada ya kutoa Historia ya Harakati za wanawake katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine wakiangalia picha ya Bibi Siti Binti Saad,iliyokuwa ikipigwa mnada katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saa,Bibi Nasra Mohamed Hilal,alipomkaribisha mlezi wa taasisi hiyo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,kuzungumza machache ili nae amkaribishe mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kutoa hutuba yake na kuizindua rasmi katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimshukuru Muharami Mohamed,Kitukuu cha Bibi Siti Bnti Saad,baada ya kumpa zawadi ya kofia aliyoivaa,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(akiyesimama) akiwa mlezi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuizindua taasisi hiyo katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Viongozi na wananchi wakati alipozindua Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisoma maandishi yanayosomeka "TAASISI YA MWANAHARAKATI BIBI: SITI BINTI SAAD"mara baada ya kufanya izinduzi wa Taasisi hiyo jana katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...