Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimpa zawadi Mwenyekiti wa Kamati ya
Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon wa Mwisho kulia
ni Mkurugenzi Mkazi Ujirani Mwema, leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya
Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon akimpa zawadi Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda , leo Mjini
Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Anna Makinda akimweleza Mwenyekiti wa Kamati ya
Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon, Mipango
mbalimbali inayofanywa na Tanzania kuimarisha uhusiano na Korea Ikiwamo
ufunguaji wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea, wakati wa kikao
kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya
Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowassa akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kamati
ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon (hayupo
pichani) wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya
Nje na Muungano kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon akimweleza Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda mpango wa kuendelea
kushirikiana na Tanzania katika masuala yatakayochangia maendeleo kwa
nchi na wananchi husika.
Wajumbe wa Kamati za Mambo ya Nje
za Tanzania na Korea wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Anna Makinda wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo
Mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward Lowasa akimweleza
jambo Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Bw.
Ahn Hong Joon (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo
Mjini Dodoma.Picha na Hassan Silayo
--
Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma
Na Jovina Bujulu, Maelezo Dodoma
Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na mpango wa kuanzisha ubalozi Tanzania Nchini Korea.
Hayo
yamesemwa leo na Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
alipotembelewa na Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano kutoka Korea Mjini
Dodoma leo.
Spika
Makinda alisema kuwa serikali itaendelea kulisimamia suala hili ikiwa
ni njia moja wapo ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
“Tuna
kila nia ya kufungua ubalozi wa Tanzania nchini Korea na hii tunafanya
tukiwa na nia ya kuendelea kuujenga uhusiano kati yetu” Alisema Spika
Makinda.
Aidha
Spika Makinda alisema kuwa bunge la Tanzania limeweka mikakati
mbalimbali ili kuliimarisha na kulifanya kuwa la kimataifa ikiwamo
kuridhia uanzaji wa bunge la kimtandano (E-parliament).
Akizungumzia
kuhusu uanzishaji wa Radio ya Bunge Spika Makinda spika alisema kuwa
bunge linampango wa kuwa na Radio ya bunge ili kupunguza gharama za
kutumia radio za taifa kama wanavyofanya sasa.
Pia
Spika Makinda alimtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano
kutoka Korea Bw. Ahn Hong Joon kushirikiana katika kuanzisha chama cha
ushirikiano cha wabunge wa Korea na Tanzania.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Muungano ambaye ni mbunge wa
bunge la Korea Bw. Ahn Hong Joon, alimuahidi Spika Makinda kuendelea
kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwamo mpango wa
Tanzania kuwa na Bunge la kimtandao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bw. Edward
Lowasa alishukuru Serikali ya Korea hasa kutokana na Misaada mbalimbali
wanayopata kutoka Serikali ya Korea ikiwamo ujenzi wa chuo cha afya na daraja la malagarasi.
FURSA ZA WAKOREA HAWA ZITUMIKE VIZURI
ReplyDeleteWAKOREA WAMEKUWA NA MSAADA MKUBWA KWA NCHIYETU
SWALI LA KUJIULIZA JE KWANINI TANZANIA TUSITUMIE RASILIMALI WATU WA TAIFA KWA AJILI YA KUSOMA ZAIDI ELIMU YA UJASIRIAMALI ILI KUZITUMIA RASILIMALI ZETU KUJIJEENGEA MIUNDO MBINU WENYEWE