Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kulia)
akiangalia jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Shirika la Reli la Tanzania na
Zambia (TAZARA) mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya shirika hilo jana jijini
Dar es Salaam kwenda kuangalia miundo mbinu ikiwemo mabehewa na injini za
treni za shirika hilo.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao
(katikati) akielekea katika moja ya treni ya Shirika la Reli la TAZARA kwa
ajili ya kuelekea katika moja ya kituo cha Mizigo cha treni ya TAZARA
kilichopo Yombo jiji Dar es Salaaam.
|
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa
amekaa ndani ya moja ya treni ya abiria tayari kuelekea katika kituo cha
Mizigo cha treni ya TAZARA kilichopo Yombo jiji Dar es Salaaam. Kulia ni
mgeni wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao.
|
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe akishuka toka ndani
ya treni ya abiria ya TAZARA kuelekea katika kituo cha mizigo cha TAZARA
kilichopo mtaa wa Yombo jijini Dar es Salaam.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao
akishuka toka ndani ya treni ya abiria ya TAZARA kuelekea katika kituo cha
mizigo cha TAZARA kilichopo mtaa wa Yombo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kupatiwa maelezo ya kina kuhusiana na reli hiyo.
|
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpa maelezo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kulia)
kuhusiana na shughuli zifanywazo na kituo cha kuhifadhia mizigo inayobebwa na
treni ya Shirika la TAZARA wakati alipotembelea katika kituo hicho jana jijini
Dar es Salaam.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (wa
pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Waziri wa
Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) mara baada ya kukamiliha ziara ya
kutemebelea Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA)jana
jijini Dar es Salaam.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto)
akimshukuru Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) mara baada ya
kupata maelezo mazuri kuhusu kazi zifanywazo na Makao Makuu ya Shirika la
TAZARA.Picha zote na Benedict Liwenga
|
No comments:
Post a Comment