Mhe.
Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania akitoa mchango wa Tanzania kwenye Kikao cha Mawaziri wa Umoja
wa Afrika. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja
wa Afrika Mhe. Naimi Aziz na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Mhe. Christopher Chiza wakifuatilia mchango huo kwenye mkutano
unaoendelea Mjini Malabo Equatorial Guinea tarehe 23-24 Juni 2014.
Mkurugenzi
wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
akifuatilia majadiliano ya vikao vya wataalam kabla ya Kikao cha
Mawaziri kuanza. Wengine pichani ni maafisa wa Mambo ya Nje Sam
Shelukindo, Elisha Suku na Zuleha Khamis.
Mhe.
Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa
kwenye mazungumzo ya faragha na Mawaziri wenzake wa Mambo ya Nje wa
Botswana (juu) Mhe. P.T.C. Skelemani na (chini) Mhe. Netumbo Nandi
Ndaitwah wa Namibia pembezoni mwa mikutano ya Mawaziri wa Umoja wa
Afrika Mjini Malabo, Equatorial Guinea tarehe 23-24 Juni 2014.
No comments:
Post a Comment