Daladala zilizochomwa moto wakati wa shambulio hilo la Mpeketoni, Lamu nchini Kenya. |
Daladala zilizochomwa moto wakati wa shambulio hilo la Mpeketoni, Lamu nchini Kenya. |
Magari yaliyochomwa moto katika kituo cha polisi cha Mpeketoni.
WATU zaidi ya 30 wameuawa, hoteli mbili, kituo cha polisi na kituo
cha mafuta kuchomwa moto baada ya shambulio lililotokea eneo la
Mpeketoni, Lamu nchini Kenya jana usiku.Kituo cha Polisi cha Mpeketoni, hoteli ya Breeze View na Taweel ndivyo vilivyochomwa moto na moshi ulikuwa bado unafuka asubuhi hii.
Imeelezwa kuwa washambuliaji walitokomea na silaha na magari ya polisi kutoka kituo hicho cha polisi baada ya kushambulia.
Awali washambuliaji hao waliteka daladala mbili 'matatu' eneo la Witu kabla ya kufanya shambulio hilo.
Wananchi walikimbilia katika nyumba zao wakati polisi wakijibizana risasi na magaidi hao ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo anadai kusikia washambuliaji hao wakisema "ambieni baba yenu atoe jeshi Somalia” wakimaanisha wamwambie Rais Kenyatta aondoe jeshi nchini Somalia.
Makundi ya Al Shabaab na MRC militia yanadaiwa kuhusika na shambulio hilo
No comments:
Post a Comment