JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
Utangulizi:
Ofisi
ya Waziri Mkuu – TAMISEMI imewapangia vituo vya kazi ya ualimu walimu
waliohitimu Vyuo vya Ualimu Mwaka 2013 kuchukua nafasi za walimu ambao
hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa kwa ajira ya Machi 2014.
Baadhi
ya waombaji hawakupangiwa vituo vya kazi kutokana na kutokuwa na sifa
zinazostahili kuajiriwa katika utumishi wa umma kwa mfano:- umri
na maombi kutoambatanishwa na vithibitisho muhimu n.k.
Maelekezo kwa Walimu Ajira Mpya
- Kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa kwa ajili ya kupangiwa vituo kuanzia tarehe 25/6/2014, hadi tarehe 30/6/2014.
- Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 30/6/2014 hatapokelewa tena na nafasi yake atakuwa ameipoteza.
- Walimu hawa ni wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi kufuatia Orodha iliyotangazwa Machi 2014 hivyo OWM – TAMISEMI haitafanya mabadiliko yeyote ya vituo katika orodha hii.
Imetolewa na: -
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA ZA MITAA NA SERIKALI
NA NURUDINI STAMBULI
No comments:
Post a Comment