Mshambuliaji wa timu ya Brazil, Neymar da Silva Santos Júnior ' Neymar '.
John Joseph na mtandaoNJIA ya kuelekea kwenye fainali ya Kombe la Dunia 2014 inachongwa leo Ijumaa na kesho Jumamosi ambapo kutakuwa na mechi nne za robo fainali.
Kiungo wa timu ya Taifa Colombia, James Rodriguez
Mechi hizo zinaaminika kuwa ngumu kutokana na uwezo wa timu husika
kutofautiana kwa kiwango cha juu, hivyo shughuli inayotarajiwa hapo
inaweza kuwa ngumu ambapo watakaoshinda wanaweza kufurahia kwa kucheza
kama vile wanacheza ile staili ya skelewu kama ya mwanamuziki wa
Nigeria, Davido.Brazil Vs Colombia
Inaaminika hi inaweza kuwa mechi nzuri kuliko zote za hatua hiyo, mechi hii ya leo pia ndiyo yenye mguso mkubwa kuliko zote kwa kuwa inahusisha wenyeji ambao wanaonekana kuwa na hasira ya kutaka kufanya kweli baada ya wachambuzi wa soka kuwakosoa kuwa uwezo wao ni wa kawaida.
Brazil ilitinga hatua hiyo kwa kuiondoa Chile kwa penalti baada ya kubanwa kwa dakika 120, wakati Colombia iliifunga Uruguay mabao 2-0 na hivyo kuonekana tishio zaidi kwa wenyeji.
Mashabiki wa timu ya Brazil.
Uwezo wa Brazil umekosolewa kuwa siyo wa kiwango cha juu kama ambavyo
ilivyokuwa kawaida ya timu hiyo miaka ya nyuma, hivyo wachezaji na
benchi la ufundi la timu hiyo wanahitaji kuuthibitishia ulimwengu kuwa
sasa wanaanza kazi.Colombia ni moja ya timu ambayo ilikuwa haipewi nafasi ya kufika mbali, lakini kadiri muda unavyosonga mbele ndivyo ambavyo wanazidi kuonekana hatari na kutishia hata amani ya wenyeji.
Brazil ndiyo ambao wapo kwenye presha kubwa kwa kuwa mashabiki wao hawataki kusikia kitu kinaitwa kufungwa, hasa kwa kuwa kulikuwa na migogoro mingi juu ya nchi yao kuandaa michuano hiyo mikubwa kuliko yote katika soka duniani.
Wazalendo wengi walipinga kufanyika kwa michuano hiyo nchini humo kwa kile walichodai kuwa serikali ilitumia fedha nyingi kuwekeza kwenye maandalizi wakati wananchi wengi hawana kitu, yaani uchumi wao upo duni.
Brazil ina madeni makubwa
Staa wa timu hiyo, Neymar hakuwa kwenye hali nzuri katika siku kadhaa zilizopita baada ya kuumia wakati wa mechi chidi ya Chile, anatakiwa kuendelea kuwa nguzo muhimu ya kulibeba taifa lake.
Wachezaji wa timu ya Colombia wakicheza Skelewu.
Pamoja na ushindi, bado Neymar hajawa chachu ya kuwafurahisha Wabrazili wengi.Timu ya taifa ya Brazil huwa inajali zaidi soka la kuvutia pamoja na ushindi, mpaka hatua iliyofikia, bado haijaonyesha ubora zaidi ya kupata ushindi kwa tabu.
Kuepusha maandamano
Wananchi waliokuwa wakipinga michuano hiyo kwa kiwango cha juu, wengi wao wamepunguza hasira kwa kuwa timu yao ya taifa inafanya vizuri, lakini ikitokea tu wakatolewa, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuibuka kwa vurugu upya.
Kocha wa Brazil, Luis Fellipe Scolari analijua hilo na ndiyo maana amekuwa kwenye presha kubwa kuhakikisha anatwaa ubingwa, hata kama Brazil haichezi soka la kuvutia.
James Rodriguez ni mtu hatari
Huyu kijana amekuwa hatari kwa wapinzani wengi, jina lake halikuwa kubwa awali, lakini kwenye michuano hiyo amekuwa namba mbaya na ndiyo maana Wabrazili wote wanatakiwa kuwa naye makini.
Rodriguez ambaye anaichezea Monaco ndiye anayeongoza kwa mabao, amefunga mabao matano na kufunika kabisa pengo la Radamel Falcao ambaye aliondolewa kikosini baada ya kuwa majeruhi.
Rodriguez siyo kwamba ana uwezo wa kufunga tu lakini pia kusaidia timu kufunga, kwani mpaka sasa amepiga pasi nne za mwisho, hiyo inaonyesha jinsi ambavyo ubora wale ulivyo juu na ndiyo maana amekuwa akiwaniwa na klabu kubwa.
Macho yote kwa Neymar
Nyota huyo wa Barcelona anatarajiwa kuanza kwenye kikosi cha leo licha ya awali kuripotiwa kuwa na maumivu ya goti, atatakiwa kuuonyesha ulimwengu kuwa yeye ni bora zaidi ya Rodriguez ambaye sasa anatajwa kuwa dsiye staa mpya wa dunia anayeinuka.
SAFARI YA BRAZIL
Kundi A
P W D L Pts
Brazil 3 2 1 0 7
Mexico 3 2 1 0 7
Croatia 3 1 0 2 3
Cameroon 3 0 0 3 0
Brazil 3-1 Croatia
Staa wa mechi: Neymar (Brazil)
Brazil 0-0 Mexico
Staa wa mechi: Ochoa (Mexico)
Cameroon 1-4 Brazil
Staa wa mechi: Neymar (Brazil)
16 Bora
Brazil 1-1 (3-2) Chile
Staa wa mechi: César (Brazil)
SAFARI YA COLOMBIA
Kundi C
P W D L Pts
Colombia 3 3 0 0 9
Ugiriki 3 1 1 1 4
Ivory Coast 3 1 0 2 3
Japan 3 0 1 2 1
Colombia 3-0 Ugiriki
Staa wa mechi: Rodríguez (Colombia)
Colombia 2-1 Ivory Coast
Staa wa mechi: Rodríguez (Colombia)
Japan 1-4 Colombia
Staa wa mechi: Martínez (Colombia)
16 Bora
Colombia 2-0 Uruguay
Staa wa mechi: Rodríguez (Colombia)
Ufaransa Vs Ujerumani
Mechi nyingine ya leo ni hii. Awali Ufaransa ilionekana kama inapata timu ambazo ni mchekea, hivyo hata wachambuzi wengi wa soka wakashindwa kuipa thamani ya ubora wa kutwaa ubingwa, lakini kadiri ilivyokuwa ikipata ushindi ndivyo ambavyo kuelewana kwa wachezaji kulivyozidi kuwa bora.
Ufaransa ilikuwa katika kundi moja na Switzerland, Ecuador na Honduras, pia ikafika hatua ya robo fainali kwa kuifunga Nigeria mabao 2-0 kwa taabu katika dakika 120, baada ya matokeo ya 0-0 kwenye dakika 90 za kawaida.
Ujerumani ilikuwa kundi lililoonekana ni gumu, kwani ilikuwa dhidi ya Ghana, Marekani na Ureno, pia ikaitoa Algeria, hivyo nayo inaonekana ipo vizuri.
Argentina Vs Ubelgiji
Argentina nayo ni kama ilivyo kwa Brazil, bado inaonekana haichezi soka la kuvutia kutokana na ina ya mastaa waliopo kikosini, hivyo Lionel Messi na wenzake wana kazi ngumu kulibeba taifa hilo kesho.
Ubelgiji wana wachezaji wengi wenye ubora wa juu lakini ambao hawajawa na uzoefu wa kufika kwenye hatua za juu katika michuano mikubwa wakiwa pamoja ndani ya timu ya taifa, hiyo haiwazuii wao kuonyesha kuwa wanaweza kufanya makubwa.
Mechi hii inatarajiwa kuwa ngumu kutokana na aina ya wachezaji wa timu zote mbili, kwani wengi wao wanachezea timu kubwa Ulaya.
Uholanzi Vs Costa Rica
Uholanzi inaundwa na mchanganyiko wa wachezaji mastaa na wengine wa kawaida, hiyo imechangia kuwa na kasi, lakini katika mechi iliyopita dhidi ya Mexico haikuonyesha uwezo mzuri, hiyo iliwachanganya wengi na kuwapa hofu juu ya wapinzani wao ambao hawana majina makubwa lakini moto wao ni hatari. Hivyo, kesho moto utawaka.
No comments:
Post a Comment