Andy Coulson wakati akifikiswa Mahakama ya Old Bailey, London leo.
Mapaparazi wakiwa kazini wakati Andy Coulson akiwa eneo la mahakama ya Old Bailey.
ALIYEKUWA mhariri wa gazeti la News of the World, Andy Coulson
amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kusikiliza mawasiliano ya watu
kwa siri. Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Old Bailey
iliyopo jijini London, England.Akitoa hukumu hiyo, jaji Justice Saunders ameiambia mahakama ya Old Bailey kuwa hiyo itakuwa fundisho kwa bwana Coulson baada ya kusikiliza mawasiliano ya watu kwa siri akiwa News of the World maana alijua kuwa ni kosa lakini akaendelea kufanya hivyo.
Gazeti la News of the World lililokuwa maarufu Uingereza na kuwa gazeti la kwanza kwa mauzo kwenye magazeti ya kiingereza duniani katika kipindi fulani, lilifungwa rasmi Julai 10, 2011.
Oktoba mwaka 2010 gazeti hilo lilikuwa likiuza wastani wa nakala 2, 812, 005 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment