Shirika la afya
duniani WHO limetangaza kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa afrika
kama janga la kimataifa linalohitaji kushughulikiwa kwa dharura.
WHO imesema kuwa mataifa yalio na
maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hayana uwezo wa kudhibiti kiwango
cha virusi hivyo na hivyo basi yanahitaji usaidizi wa kimataifa.Tangazo hilo linajiri baada ya mazungumzo ya dharura mjini Geneva kuhusu uwezekano wa kutuma wataalam wa ugonjwa wa maambukizi ili kuudhibiti ugonjwa huo ambao ni hatari zaidi.
Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu mia tisa magharibi mwa afrika .
Mataifa yalioathiriwa vibaya ni Guinea,Liberia na Sierra Leone,lakini pia visa vimeripotiwa nchini Nigeria.
bbc
No comments:
Post a Comment