MESSI AVUNJA UKIMYA ACHUKUA JIKO RASMI
Usiku wa Ijumaa ya June 30 staa wa soka wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi alifunga ndoa na mpenzi wake wa toka utotoni Antonella Roccuzzo ambaye pia wamezaa nae watoto wawili wa kiume. |
Messi na Antonella Roccuzzo walifahamiana toka Lionel Messi akiwa na umri wa miaka mitano na Antonella Roccuzzo ambaye ni mke wake kwa sasa akiwa na umri wa miaka 4, wameamua kufunga ndoa kwao Argentina ndoa ambayo ilihudhuriwa na wachezaji wenzake na marafiki zake mbalimbali.
Zaidi ya marafiki wa Lionel Messi wanaofikia 250 walisafiri kwa ndege binafsi kuelekea Argentina kuhudhuria harusi ya staa huyo ambayo simu za mkononi zilikuwa zimefungiwa kufanya kazi ndani ya ukumbi sherehe ilipo kwa lengo la kuweka privacy pamoja na ulinzi wa askari zaidi ya 450.
No comments:
Post a Comment