Mkurugenzi
wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo
Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (wapili kulia) akimkabidhi Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye tuzo ya
cheti cha heshima, kwa mchango wao katika kupambana na majanga ya moto
na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar
es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akionesha
zawadi ya fulana ya mabalozi wa Taasisi ya Salama Salimini
aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa
Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani
(kushoto), kama alama ya kutambua mchango wao katika kupambana na
majanga ya moto na uokoaji, (kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi
Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es
Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akifafanua
jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa
tuzo ya cheti cha heshima kutoka kwa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa
Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), kwa mchango wao
katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika
Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa tatu
kulia) akiwa na Viongozi Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi wa
Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo
Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (wapili kushoto), (kulia) Kamishna
wa Operesheni wa Jeshi hilo Billy Mwakatage, (kushoto) Kamishna wa
Usalama Dhidi ya moto Jesuald Ikonko na (wapili kulia) ni balozi wa
Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya
Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)
NA MWANDISHI WETU NURUDINI STAMBULI
Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua
mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini
kutoka katika Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo. Tuzo hiyo imepokelewa
na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye
Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es salaam
Akizungumza
Kamishna Jenerali baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho. Alisema,
anawashukuru Taasisi hiyo kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi
nyingi ambazo taasisi hiyo imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo
ikiwepo kampeni ya kuitangaza namba ya simu ya dharura 114.
Kamishna
Jenerali Andengenye, amezitaka Taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi
hilo katika kuzifufua Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili
kuongeza idadi ya vifaa hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga
ya moto. ‘‘Jamii ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo
(Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya
moto yanapotokea’’.
Ni
vema sasa mamlaka zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye
miji na majiji ikazingatia wanapotengeneza miundo mbinu hiyo, wakumbuke
kuweka na mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha
wamiliki wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya
maji.
Tuna
changamoto kubwa kwa upande wa visima hivyo, kwa hiyo kamapeni yetu ya
kufufua na kuongeza visima hivyo vitasaidia kuleta tija katika utendaji
kazi katika fani yetu. Tunashirikiana na Mamlaka za Maji kuhakikisha
miundo mbinu hiyo inarudi na kutoa ushauri pale miradi mipya ya maji
inapo jengwa.
Naye
Mkurugenzi wa Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania Bw. Muhammad
Shaban alisema wamechukua uamuzi huo wa kutoa Tuzo hiyo kutokana na
kuona mchango mkubwa wa Jeshi hilo walioutoa katika jamii. Pia amesema
wataendea kutoa ushirikiano na Jeshi hilo katika utoaji elimu kwa umma.
“Tupo tayari kushirikiana na Jeshi hili kuwaonesha sehemu zote ambazo
fire hydrant zilizopo Mkoa wa Dar es salaam.”
“Kampeni
ya kufufua fire hydrant imetugusa sana na kuona hatua hiyo ni msaada
mkubwa kwa jamii kwani zitasaidia magari ya zimamoto na uokoaji kupata
maji eneo la karibu majanga ya moto yanapotokea.”
No comments:
Post a Comment