Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Iddi (wa tatu kushoto) akifurahia pamja
na Nahodha wa timu ya Azam Fc, Himid Mkami na Jabir Aziz, baada ya kuwakabidhi
zawadi ya kitita cha fedha taslimu Sh. Milioni 10, na Kikombe cha ushindi baada
ya kuifunga timu ya Tusker ya Kenya kwa mabao 2-1, katika mchezo wa Fanali ya
Kombe la Mapinduzi zilizofikia tamati, jana Januari 12, huku mshindi wa pili wa
mashindano hayo, Tusker ya Kenya wakijipatia kiasi cha Sh. Milioni 5 na Kikombe
cha mshindi wa pili, na zawadi ya mfungai Bora wa michuano hiyo alikuwa ni
Mchezaji wa Tusker ya Kenya, Jese Wele, aliyejinyakuliwa Sh. 300,000.

Mchezaji
wa Azam Fc. Gaudance Mwaikimba (katikati) akiruka kuwania mpira na kipa wa
Tusker ya Kenya, Samuel Odhiambo, wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi. Bao
lililofungwa na Mwaikimba katika Dakika ya 93 ndani ya muda wa dakika za
nyongeza, liliiwezesha timu hiyo kuwa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya
pili mfululizo.
Mwaikimba,
akikosa bao la wazi......., Katika mchezo huo timu ya Tusker ndiyo ilikuwa ya
kwanza kujipatia bao lililofungwa na Jese Wele, katika Dakika ya 60, na baadaye
Azam waliweza kusawazisha bao hilo kupitia kwa Beki wake, Jockins Attudo, kwa
njia ya penati katika dakika ya 72, baada ya mchezaji mmoja wa Tusker kuunawa
mpira katika eneo la hatari kufuatia shuti kali lililopigwa na Khamis
Mcha.
Beki na
Nahodha wa Azam, Himid Mkami, akijipinda kupiga shuti wakati akiokoa moja ya
hatari zilizoelekezwa langoni kwake.
Kipa wa
Tusker ya Kenya, Samuel Odhiambo, akigaa gaa chini, baada ya kushindwa kuokoa
mkwaju wa penati, iliyopigwa na Attudo.
Shughuli
ilikuwa pevu kati ya Mwaikimba na Shikokoti, Hapa Mwaikimba akijipinda kuachia
shuti ambalo hata hivyo halikuweza kuzaa matunda.
'KITUKO
UWANJANI' Aidha katika mchezo huo kilizuka kituko cha mwaka, baada ya mwanadada
huyu aliyevalia ushungi kukatiza katikati ya uwanja wakati mchezo ukiendelea,
jambo ambalo lilimfanya mwamuzi wa mchezo huo, kusimamisha mchezo na kumfuata
ili kujua kulikoni. Hapa ni wakati akilia denge ili amzuie asikatize uwanjani,
lakini hakufanikiwa kwani kila alivyojitahidi kumsihi mdada huyo, hakusikilizwa
ila mdada huyo aliendelea kwenda kuelekea kukatiza uwanjani hapo, jambo ambalo
lilizua hisia nyingine miongoni mwa mashabiki wa soka waliokuwepo uwanjani hapo
huku, yakisikika makelele ya mshangao kutoka majukwaani.
Mwamuzi
akizungumza na mdada huyo huku akitumia busara kumsindikiza nje ya
uwanja....
Bado
hakijaeleweka....
Mwamuzi
huyo baada ya kuona amemfikisha salama na kuvuka alama ya mstari wa mwisho wa
uwanja, alianza kuomba msaada wa askari ili kumtoa binti huyo
uwanjani.
Binti
huyo akiwa tayari chini ya ulinzi wa polisi, huku akisindikizwa na Msemaji wa
Kamati ya Maandalizi ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Farouk
Kareem.
Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akimkabidhi zawadi ya Kombe la
mshindi wa pili, Nahodha wa Timu ya Tusker kutoka Kenya, Joseph Shikokoti, baada
ya timu yake kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam, katika mchezo
uliochezwa kwenye Uwanja wa Amani, mjini Zanzibar jana usiku.
Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akimkabidhi zawadi ya Sh.
300,000, mfungaji bora wa mashindano hayo, Jese Wele.
Gaudance
Mwaikimba, akifurahia kombe na mashabiki wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment