
Naibu waziri wa elimu mh.philipo mulugo amewatoa hofu walimu wanaotarajia kupangwa katika vituo vya kazi kwa kuwaomba kuwa na subira kwani ndani ya wiki hii watajua ni wapi wamepangwa huku akisisitiza walimu wote watapangwa vijijini ambapo kumekuwa na tatizo la upungufu wa walimu,Mh.mulugo ameyasema hayo katika kipindi cha jambo tanzania kinachorushwa kupitia televisheni ya taifa TBC 1,amesisitiza wakurugenzi wa halmashauri kuwapokea vizuri walimu hao mara watakaporipoti katika halmashauri zao huku akisisitiza walimu watalipwa pesa za kujikimu kwa awamu na hakuna mwalimu ambae atakosa haki yake.
No comments:
Post a Comment