
Janeth huenda akapata utajiri wa dola $500 million endapo ndoa hiyo itavunjika kwa muda wa chini ya miaka mitano toka kufungwa ambayo inatarajiwa kufanyika mapema mwaka huu. Taarifa hii imekuja baada ya mwanamuziki huyo kutoa habari kupitia vyombo vya habari tofauti na kueleza mikakati ya kufunga ndoa yao hiyo ambayo inasubiriwa na watu wengi.
Ndoa hiyo ambayo ilitakiwa ifanyike mwaka jana baada ya wakili wa pande zote mbili kuchelewa kukamilisha nyaraka zote za pande mbili tofauti za mkataba wa ndoa yao pamoja na baada ya kufunga ndoa hiyo. Hata hivyo haijawekwa wazi ni siku gani ndoa hiyo itafungwa rasmi.
No comments:
Post a Comment