airtel

airtel

.

.

Tuesday, January 15, 2013

MAN WAALTER: NIMEMSAMEHE 20 PERCENT,TURUDI KAZINI NA TUNYANYUE MZIKI WETU


     Producer wa muziki maarufu nchini, Man Walter [Pichani, Kushoto] atangaza kumaliza beef zake zote alizokuwa nazo na wasanii. Akizungumza na radio moja maarufi nchini, Man Walter alizungumza kumaliza matatizo yote aliyokuwa nayo na wasanii ikiwemo hata yale ambayo hayajui...
     Akizungumzia kuhusu 20%, Man Walter alisema beef yake na 20% ni moja ya matatizo ambayo yalikuwepo na sasa hayataki tena, yuko tayari kufanya kazi na msanii wowote ikiwemo 20%.
     Akiongelea beef zingine, Man Walter alisema wapo wasanii au watu ambao unaweza kuwa na matatizo nao bila kujua, mtu ana beef na wewe ya kichini chini lakini mimi nimeyamaliza yote.
Kipindi fulani nyuma, producer Man Walter aliingia kwenye beef na 20% na kushindwa kuendelea kufanya kazi na msanii huyo ambaye wamefanya kazi nyingi pamoja.
Nasta boy blogspot inampongeza man walter kwa moyo wa usamehevu na unamtakia kazi njema za  kuwainua wasanii wetu wa hapa nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...