Mamilioni ya waumini wa madhehebu ya Hindu nchini India wamejitosa katika mto wao mtakatifu wa Ganges, kitendo ambacho wanaamini kinawaosha dhambi zote.
Siku ya
leo inachukuliwa kama siku yenye heri kubwa zaidi katika maadhimisho ya
siku 55 yajulikanayo kama Kumbh Mela, ambayo umuhimu wake unatokana na
masuala ya kinajimu.
Afisa
Mkuu wa maadhimisho hayo Mani Prasad Mishra amesema tayari watu milioni
tatu wamekwishaingia ndani ya mto Ganges kuanzia asubuhi na kwamba
wanategemea kuwa ifikapo jioni watu milioni kumi na moja watakuwa
wamejiosha na maji ya mto huo yenye baridi kali.
Wakereketwa
wa dini ya Hindu wanaamini kwamba kuoga ndani ya mto Ganges kunaondoa
dhambi zao, na kuwaepusha na mzunguko wa kifo na kuzaliwa kwa mara ya
pili.
No comments:
Post a Comment