Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kama ishara ya
kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya
Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la
matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya
Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.
Makabidhiano hayo yamefanyika
katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na
kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.

Afande Inspekta Mkweru akijaribu moja ya pikipiki zilizokabidhiwa leo kwa maafisa wa jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya makabidhiano hayo makao makuu
ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo asubuhi, katikati ni
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman
Kova
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi
la Polisi Paul Chagonjaakizungumza jambo na Msemaji wa Jeshi la Polisi
nchini Tanzania Advera Senso wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa maafisa hao wa polisi leo
No comments:
Post a Comment