KWA UFUPI
ATCL
ilisitisha safari zake April 9, 2012 baada ya ndege yake aina ya Dash 8
kupata ajali katika kiwanja cha Kigoma, hivyo Shirika hilo kukosa ndege
nyingine. Miezi miwili iliyopita shirika hilo lilinunua ndege mpya.

ABIRIA 25 waliokuwa wakisafiri na ndege
ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam
wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kupata ufa
katika kioo cha mbele, hivyo kumfanya rubani abadili mwelekeo na kutua
kwa dharura uwanja wa ndege wa Kigoma.
Tukio hilo lilitokea juzi jioni muda
mfupi baada ya ndege hiyo aina ya Bombadia Dash 8 kuruka katika uwanja
wa ndege wa Kigoma, ikiwa katika safari zake za kwanza, baada ya
kusitishwa takriban miezi tisa iliyopita.
ATCL ilisitisha safari zake April 9,
2012 baada ya ndege yake aina ya Dash 8 kupata ajali katika kiwanja cha
Kigoma, hivyo Shirika hilo kukosa ndege nyingine. Miezi miwili iliyopita
shirika hilo lilinunua ndege mpya.
Kaimu Mkurugenzi wa ATCL, Kapteni Milton
Lazaro alisema ilipata hitilafu hiyo dakika 15 tangu iliporuka, baada
ya kioo cha mbele kupata ufa.“Ufa ule uliwatisha marubani na waliamua
kutua kwa dharura kwa sababu kioo kingeweza kupasuka na kusababisha
ajali mbaya na ndege kuanguka,” alisema Lazaro na kuongeza;
“Kawaida vioo vya ndege hupashwa moto
ndege inapoondoka na endapo utatokea ufa wowote ni lazima irudi
kiwanjani na kama ipo mbali na kiwanja inambidi rubani ateremke chini na
kupunguza mwendo.”
No comments:
Post a Comment