airtel

airtel

.

.

Saturday, February 2, 2013

KAULI YA WEMA SEPETU BAADA YA KUMPULIZIA MBWA WAKE PERFUME YENYE THAMANI YA DOLA 120

“Lazima anukie kama mimi ninavyonukia, pafyumu humfanya anukie vizuri hata ninapokuwa nimetoka naye mitaani naye anaonekana kweli ni mbwa wa staa,” alisema Wema.
Kuhusu manunuzi, mkali huyo anayekimbiza kwenye soko la filamu Bongo alisema mara nyingi pafyumu hizo huwa anaagiza kutoka nje au kwa watu wake maalum hapa Bongo ili kuwa na utofauti wa ubora na hadhi yake ya kistaa.
Wema aliendelea kusisitiza kuwa mbwa huyo huwa anampa kampani na wakati mwingine humfurahisha pindi anapokuwa ameboreka au anapokuwa peke yake nyumbani.
“Mara nyingi huwa naagiza kutoka Uarabuni, unajua kule pafyumu zao ni nzuri na ubora wake ni wa hali ya juu,” alisema Wema.
Mkali huyo mara nyingi amekuwa akitumia pafyumu za kuanzia dola 300 (shilingi laki nne na nusu) na kuendelea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...