[Football] Yaya Toure Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Africa Mara 3 …
Mara baada ya masaa 24 kupita tokea timu yake ya klabu ya Manchester
City kufanikiwa kuisambaratisha timu ya West Ham United kwa mabao 6 kwa
0 katika mashindano ya Capital One Cup huko Uingereza, mchezaji mpira
mahiri wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Manchester City ya Uingereza
amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Africa kwa maara ya tatu
mfululizo, ambapo mahafali hayo yalifanyikia katika ukumbi wa Gala
nchini Nigeria katika jiji kubwa la Lagos.

Kutokana na kiwango cha mchezaji huyo wa kati wa timu ya Man City na
Ivory Coast, ambacho kimekuwa juu kwa muda mrefu ni sababu iliyomfanya
mcezaji huyo kutwaa tuzo hiyo na pia mchango wake wakuweza kuifanikisha
timu yake ya Taifa kufuzu kucheza mashindano ya World Cup
yatakayofanyika South America Brazil. Wachezaji wengine waliofanikiwa
kutwaa tuzo hiyo mara tatu mfululizo ni Abedi Pele wa Ghana na Samuel
Etoo wa Cameroon ambapo Etoo alichukua 2003-05 na kuchukua kwa mara ya
nne 2010.
No comments:
Post a Comment