airtel

airtel

.

.

Tuesday, September 9, 2014

MV KIGAMBONI KUREJEA ALHAMISI HII BAADA YA MATENGENEZO MAKUBWA YA WIKI TATU.


Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli  akiongea na wajumbe mbalimbali waliofika katika  uzinduzi wa kivuko cha kigamboni  leo jijini Dar es  Salaam kinachofanyiwa matenganezo  na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini ,ambacho kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi alhamisi wiki hii.

Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati mwenye suti nyeusi) akielekea katika eneo  ambalo kivuko cha MV Kigamboni  kilipo kwa ajili ya ukaguzi wa kazi iliyofanywa na wahandisi wa Jeshi la Wanamaji leo jijini Dar es Salaam.

Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana  upande wa mbele na ubavuni , kikiwa katika hatua za mwisho tayari kwa kuanza  kutumiwa na wananchi siku ya alhamisi baada ya matengenezo yaliofanywa na Jeshi la Wanamaji  kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.

Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo kutoka kwa  Msimamizi wa matengenezo  Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kulia), kushoto  ni  Mkuu wa Jeshi la Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam ,amabapo  kinatarajiwa kuanza kutumika wiki  kurahisisha usafiri kwa watu wa  Kigamboni

Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana kwa ndani, kinatarajiwa kuanza kutumika siku ya alhamisi baada ya matengenezo yalifanywa na Jeshi la Wanamaji  kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.Picha na Lorietha Laurence

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...