
Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka akiongea wakati
wauzinduzi wapromosheni ya Coke Studio msimu wa pili ambapo watejawa…

Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa
akiongea wakati wauzinduzi wa promosheni ya Coke Studio msimu wa pili
ambapo wateja wa Coca-Cola watajipatia muda wa maongezi wa dakika tano
bure kwa kila soda moja ya chupa ya Coca-Cola.
![]() |
Mwandishiwa TBC akisoma namba kutoka kwenye kizibo cha chupaya Coca-Cola wakati wauzinduzi wa promosheni ya Coke Studio msimu wa pili ambapo wateja wa Coca-Cola watajipatia muda wa maongezi wa dakika tano bure kwa kila soda moja ya chupa ya Coca-Cola |
Nae Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa akizungumza katika uzinduzi huo amesema promosheni hii inayojulikana kama Kunywa Coke #Kula5 ina lengo la kuwafurahisha wateja wa Vodacom Tanzania na wenzao wanaowazunguka. ''mteja atakuwa anafurahia kunywa Coke wakati huo pia anapata fursa ya kutumia huduma za mtandao kwa dakika 5 kwa namna yoyote anayotaka yeye (mteja) ikiwa ni kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi au kuperuzi’’
"Mteja wa Vodacom ataunganishwa na huduma hii kwa kupeleka ujumbe wenye namba iliyopo chini ya kizibo cha soda yake ya Coca-Cola ya chupa kwenda namba 15441 bila kutozwa gharama yoyote na baada ya hapo atapokea ujumbe wa uthibitisho kwamba ana dakika 5 kuanzia muda huo kutumia kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi na kuperuzi.''
Kupitia promosheni hii wateja na watanzania kwa ujumla pia watapata fursa ya kushuhudia wanamuziki mastaa wa hapa nchini wakishirikiana na wanamuziki wengine Afrika katika msimu wa pili wa kipindi cha Coke Studio Afrika kinachorushwa na Televisheni ya Taifa(TBC1 na TBC2) kila siku za Jumamosi saa 3 usiku.
Aliongeza kuwa promosheni hii inapatikana kwa wateja wa Vodacom Tanzania nchi nzima.
HABARI NA NURUDINI STAMBULI.
No comments:
Post a Comment