airtel
.
Thursday, December 25, 2014
MBUNGE WA JIMBO LA TANGA ALHAJ DR.OMAR NUNDU APIGANIA VIJANA NA AKINA MAMA WAKOPESHWE FEDHA ZA HALMASHAURI ZINAZOTENGWA KUTOKANA NA MAPATO YA NDANI YA MKOA WA TANGA
TANGA ZINDABHAA
Mbunge wa jimbo la TANGA MJINI MH.ALHAJ DR.OMAR NUNDU AMEITAKA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA INAWATENGEA VIJANA NA AKINA MAMA PESA ZA HALMASHAURI ZILIZOTAKIWA ZITENGWE KUANZIA MWAKA 1993 AMBAPO KWA MKOA WA TANGA ZIMETOLEWA MIAKA MITATU TU HUKU MIAKA 18 ILIYOFUATA ZIKIWA HAZITOLEWI NA AU KUTOKUTENGWA KABISA.
MH.NUNDU AMBAE ANATUMIA AHADI YA 4 NA 8 ZA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA KULIENDESHA JIMBO LA TANGA AMEWATAKA VIJANA KUTOKUDANGANYWA KUWA YEYE NDIE ANAYEZUIA MIKOPO HIYO ISITOKE BADALA YAKE AMEWATAKA VIJANA NA AKINA MAMA WA MKOA WA TANGA KUCHANGAMKIA FURSA HIYO AMBAYO NI YA KILA KIJANA BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA.
MH.NUNDU ALIFIKA MBALI SANA KWA KUWATAKA VIJANA WAJIJENGEE KUAMINIKA MARA WATAKAPOPATA MIKOPO HIYO KWA KUHAKIKISHA WNAITUMIA KWA MALENGO.
IKUMBUKWE MBUNGE OMAR R.NUNDU ALISAMEHE MSHAHARA WAKE WA MIAKA MITANO ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 111 KWA KUWAKOPESHA WAKAZI WATANGA ILI WAJIKWAMUE KIUCHUMI NA WAONDOKANE NA LINDI LA LA UMASIKINI ULIOP[O MKOANI HAPA,PAMOJA NA JUHUDI HIZO PESA HIZO ZILIRUDI MILIONI NANE NA IDADI KUBWA YA WALIOKOPESHWA WAKISHINDWA KUZIRUDISHA KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI IKIWEMO WATU WANAOPITA WAKISEMA PESA ZA MBUNGE HUYO ZILIKUWA ZA MISAADA.
MBUNGE OMAR NUNDU ANABAKI KUWA MBUNGE WA KWANZA KATIKA HISTORIA YA MKOA WA TANGA KUSAMEHE MSHAHARA WAKE KWA AJILI YA KUWAKOMBOA WANANCHI.
SOURCE; JAMII FORUM JUKWAA LA SIASA
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment