Mgombea
Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasha
mshumaa baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa,
Hayati Mwalimu Nyerere, Mwitongo, Butiama mkoani Mara leo.
Mama
Samia akishiriki kuomba dua kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Hayati
Mwalimu Nyerere, kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara.
Mama
Samia akiondoka baada ya kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu
Nyerere. Butiama mkoani Mara. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Msafara
wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan
ukiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambako
alika kusalimia familia hiyo na kuzuru kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere, leo, katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama, akiwa kaika ziara ya
kufanya mikutano ya kampeni katika mkoa wa Mara.
Mgombea
Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia
mtoto wa sita wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, Madaraka
Nyerere, alipowasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa huyo, katika
Kijiji cha Mwitongo, Bitiama mkoani Mara.
Mama Samia akisalimia wanafamilia wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere
Mama Samia akisalimia wanafamilia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
Chifu
wa Ukoo wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, Japhet Wanzagi,
akimkaribisha na kutoa utambulisho kwa Mgombea Mweza wa Urais Mama Samia
Suluhu Hassan,
Aliyekuwa
Muomba nia ya kugombea Ubunge jimbo la Nkenge, Asupta Mshama, akipozi
kwenye baadhi ya miamba ya mawe iliyopo katibu na kaburi la Baba wa
Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere, katika Kijiji cha Mwsenge, Butiama mkoani
Mara.
No comments:
Post a Comment